Kumuomba Allaah kwa jina la mpenzi

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema wakati wa kuomba du´aa “Ee mpenzi” (يا حبيبي) akimkusudia Allaah?

Jibu: Hakuna neno. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye mpenzi zaidi kwake. Lakini amuombe kwa majina Yake kama vile Allaah au Mwingi wa huruma (ar-Rahmaan) ndio bora zaidi. Kwa sababu Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا

”Allaah ana majina mazuri mno. Hivyo basi muombeni kwayo.”[1]

Hakusema aombwe kwa jina la mpenzi. Muombe kwa majina na sifa Zake kama vile Allaah, Mwingi wa huruma na Mwenye utukufu mno na ukarimu (Dhul-Jalaal wal-Ikraam). Ijapokuwa yeye ndiye mpendwa zaidi. Lakini muombe kwa majina Yake aliyoyaweka wazi (Subhaanahu wa Ta´ala).

[1] 07:180

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-is-Shubuhaat, uk. 112
  • Imechapishwa: 17/08/2019