Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

13- Abu Hamzah Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) mtumishi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza kwamba Mtume amesema:

“Haamini mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake kile anachojipendelea juu ya nafsi yake.”

Kumpendelea mema ndugu yako katika mambo ya kidunia kama unavyojipendelea juu ya nafsi yako, hili ni jambo limependekezwa. Ampendelee ndugu yake naye awe na mali kama jinsi anavyojipendelea juu ya nafsi yake. Hili ni jambo limependekezwa. Ampendelee ndugu yake awe na cheo kama yeye. Hili pia ni jambo limependekezwa. Bi maana ikiwa hakufanya hivo hakukanushwi ukamilifu wa imani ambako ni wajibu. Kwa sababu mambo kama haya yamependekezwa.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 221
  • Imechapishwa: 17/05/2020