Swali: Je, ni wajibu kwa mzazi kumuamsha mtoto wake wa kiume ambaye ana miaka saba ili aende kuswali swalah ya Fajr msikitini?

Jibu: Ndio. Anatakiwa kwenda nae msikitini ili amlee juu ya swalah na juu ya kheri. Ndio malezi mazuri. Asimwache kitandani; haya ni malezi mabaya. Hapa atakuwa amemfanyia ghushi mtoto wake. Yeye anachotaka ni kuwa mzuri kwake na kumhurumia, lakini  uhakika wa mambo ni kwamba amemfanyia ghushi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (81) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-16-2-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2018