Kumchukua video maiti kwa ajili ya kukumbusha watu mauti


Swali: Ni ipi hukumu ya kumchukua picha maiti kwenye kanda ya video kisha mtu akauza kwa hoja kwamba anataka kuwakumbusha watu kifo?

Jibu: Ikiwa anakusudia kumchukua picha maiti wakati anapooshwa ni jambo ambalo halijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuchukua picha viumbe vyenye roho na amemlaani mtengeneza picha pale aliposema:

“Ndio watu wataokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah.”

Lakini ikiwa malengo ya muulizaji ni kutaka kubainisha namna anavyooshwa maiti kama Allaah alivyoweka katika Shari´ah katika kanda itakayotawanywa au kuuzwa hapana vibaya. Ni kama ambavo kunarekodiwa kuwafunza watu swalah na mengineyo miongoni mwa yale mambo ambayo watu wanayahitajia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (08/425)
  • Imechapishwa: 06/07/2021