Kumchukua Khatwiyb video camera wakati wa Khutbah


Swali: Mtu anamchukua picha Khatwiyb katika Khutbah ya ijumaa. Je, kitendo chake hichi kinafaa upande wa Shari´ah kwa njia ya kunyamaza na mtu kutojishughulisha na chochote?

Jibu: Haijuzu kwao kufanya hivi. Kufanya harakati wakati wa Khutbah haifai isipokuwa kwa dharurah. Kutikisika kwa sababu ya dharurah ni sawa. Ama kutikisika pasi na dharurah wakati wa Khutbah ni kitu hakifai. Kwa sababu kinachotakikana ni kunyamaza na kujishughulisha na kusikiliza Khutbah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/18355
  • Imechapishwa: 11/04/2020