Kumchezea shere anayefuga ndevu na kufupisha nguo


Swali: Ni jambo lenye kudhihiri katika jamii nyingi za Kiislamu kuchezea shere nembo za dini za wazi ikiwa ni pamoja na kufuga ndevu na kufupisha nguo. Je, mfano wa haya yanaingia katika uchezaji shere unaomtoa mtu nje ya dini? Ni nini unachomnasihi ambaye ametumbukia ndani ya kitu kama hicho?

Jibu: Hapana shaka kufanya istihzai kwa Allaah, Mtume Wake, Aayah, Shari´ah na hukumu Zake ni miongoni mwa jumla ya aina za ukafiri. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ

“Sema:  Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayah Zake na Mtume Wake?”  Msitoe udhuru; mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.”[1]

Kunaingia katika hayo kucheza shere kwa Tawhiyd, swalah, zakaah, swawm, hajj na hukumu nyenginezo za dini ambazo kuna makubaliano juu yake.

Kumchezea shere ambaye anafuga ndevu zake, anafupisha nguo yake na mengineyo ambayo pengine hukumu zake ni zenye kufichikana yanahitaji kupambanuliwa. Ni lazima kutahadhari kufanya hivo na kumnasihi ambaye anajua kitu katika hayo ili aweze kutubu kwa Allaah na alazimiane na Shari´ah Yake. Anatakiwa kutahadhari kumchezea shere ambaye ameshikamana na Shari´ah kwa ajili ya kumtii Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtu huyo atahadhari na hasira na adhabu ya Allaah na kuritadi kutoka nje ya dini yake pasi na yeye kuhisi hilo.

[1] 09:65-66

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (07/45)
  • Imechapishwa: 11/06/2021