Kulipa siku za Ramadhaan katika Rajab


Swali: Natarajia mtanifunza miezi ambayo natakiwa kulipa masiku ya Ramadhaan ambayo sikujaaliwa kuyafunga. Ni zipi nguzo za imani? Vipi muislamu atakuwa ni muislamu bila dhambi? Mimi nina ndugu ambaye hakufunga masiku ya mwisho ya Ramadhaan tarehe 25, 26, 27, 28, 29 na 30 na anataka kuyafunga Rajab. Mnaonaje?

Jibu: Ni wajibu kwa ndugu yako kulipa masiku ambayo aliacha kufunga katika Ramadhaan. Bora zaidi ni kuwahi kuyalipa punde tu baada ya Ramadhaan kwisha isipokuwa tu kukiwa na udhuru. Nduguyo kuyalipa katika Rajab ni jambo linafaa.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alifta.net/Fatawa/FatawaChapters.aspx?languagename=ar&View=Page&PageID=344&PageNo=1&BookID=12
  • Imechapishwa: 22/03/2018