Kukumbuka Tasmiyah katikati ya wudhuu´ au baadaye


Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye amesahau kusema “Bismi Allaah” kabla ya kutawadha na akakumbuka katikati ya wudhuu´ au baada yake?

Jibu: Tasmiyah sio wajibu. Hadiyth zilizopokelewa juu yake ni dhaifu. Ibn Hajar (Rahimahu Allaah) amenukuu kutoka kwa Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ya kwamba amesema katika kitabu chake “Buluugh-ul-Maraam”:

“Hakukuthibiti katika mlango huu kitu.”

Kujengea juu ya hili endapo mtu atasema ndio bora zaidi. Vinginevyo hakuna neno. Mtu akisahau kusema mwanzoni mwa wudhuu´ aseme hivo pale atapokumbuka hata kama itakuwa ni katikati ya wudhuu´. Akimaliza kutawadha na asikumbuke hana juu yake kitu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/825
  • Imechapishwa: 05/03/2018