Swali: Je, inajuzu kuchukua mkopo katika kampuni ambapo nafanya kazi ili niweze kutekeleza Hajj ya faradhi?

Jibu: Haikulazimu kuchukua madeni kwa ajili ya Hajj. Huna juu yako Hajj. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Amesema:

وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا

”Na kwa ajili ya Allaah ni wajibu kwa watu watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo.” (03:97)

Asiyeweza hana juu yake Hajj na sio lazima kuingia katika madeni. Huku ni kujikalifisha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (55) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1432-10-13.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014