1- Kukodesha watu wasome Qur-aan na kumtumia thawabu zake maiti na kuchukua ujira juu ya kile kisomo. Jambo hili – na Allaah ndiye anajua zaidi – halijuzu pasina tofauti. Bali ni kitendo cha Bid´ah kwa kuwa hakikuelekeza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wala hakikufanywa na yeyote katika Salaf na wala hakikuamrishwa na yeyote katika maimamu wa dini. Kuchukua ujira kwa dhati ya kisomo haijuzu pasina tofauti. Kwa sababu kisomo cha Qur-aan ni ´ibaadah na ´ibaadah hakuchukuliwi ujira juu yake. Mfano wa mambo haya ni hajj, swalah na adhaana. Huyu ambaye amechukua ujira wake hakufanya ´ibaadah yake kwa Ikhlaasw. Hivyo hana thawabu zozote za kumtumia maiti. Kujengea juu ya hili hakuna yeyote aliyesema kuwa [inafaa] kuteua mtu wa kumfungia na kumswalia na kumtumia thawabu zake maiti kwa sababu yule aliyechukua ujira wake hana thawabu zozote. Vipi atamzawadia kitu kisichokuwa na thawabu?

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (02/721)
  • Imechapishwa: 19/05/2020