Kukhutubu kwa kukaa au kwa kusimama?


Swali: Je, Sunnah ni Khatwiyb kusimama katika Khutbah ya ´Iyd au inasihi kwake kukaa?

Jibu: Sunnah, sawa katika Khutbah ya ijumaa na Khutbah ya ´Iyd, ni Khatwiyb akhutubu amesimama. Hivo ndivo ilivyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)[1].

[1] al-Bukhaariy (978) na Muslim (861).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (16/247)
  • Imechapishwa: 14/06/2018