Swali: Siku ya ijumaa kuna watu waliswali sehemu ya nyuma ya msikiti. Baada ya imamu kuwaswalisha Rak´ah ya kwanza umeme ukakatika na hawakumsikia imamu. Mmoja katika maamuma akatangulia mbele na akaendelea kuwaswalisha. Ni ipi hukumu katika hilo?

Jibu: Hili ni sahihi. Midhali wamewahi Rak´ah moja pamoja na imamu basi wakamilishe Rak´ah nyingine. Wakimtanguliza mmoja wao hakuna neno. Hili ni jambo zuri. Lakini endapo wasingeliwahi Rak´ah moja pamoja na imamu, katika hali hiyo tunawaambia kwamba wangelitakiwa kutoka na kuswali pamoja na imamu ijapokuwa itakuwa ni kwenye barabara. Jengine wanaloweza kufanya ni kumteua mtu ambaye anasikia Takbiyr ya imamu na yeye awasikilizishe au kwa msemo mwingine awafikishie. Kwa sababu katika hali kama hii hawawezi kuikamilisha swalah yao ikiwa ni ijumaa kwa sababu hawakuwahi Rak´ah moja. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuwahi Rak´ah moja katika swalah basi ameiwahi swalah.”

Ikiwa hawawezi kuikamilisha kama ijumaa basi ni lazima wajaribu kuikamilisha kama ijumaa pamoja na imamu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (46) http://binothaimeen.net/content/1062
  • Imechapishwa: 03/05/2019