Kukanyaga juu ya godoro lililokojolewa na mtoto

Swali: Mimi nina watoto wadogo ambao wanakojoa kwenye godoro. Lakini baada ya kupita wakati mkojo huu unakauka na hakubaki athari yako yoyote. Je, inajuzu kwa ambaye ametawadha kukanyaga juu ya godoro hili?

Jibu: Kukanyaga juu ya godoro najisi ikiwa godoro hili wala miguu haiko unyevunyevu haidhuru na wala haithiri… Lakini miguu ikiwa na unyevunyevu na sehemu hiyo ikawa najisi, basi ni wajibu kuosha miguu baada ya hapo.

Lakini mimi nawanasihi ndugu zangu godoro likipatwa na najisi basi waharakishe kulisafisha. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndivo alivokuwa akifanya ambapo anakimbilia kuosha najisi. Wakati mbedui yule alipomaliza kukojoa ndani ya msikiti, papo hapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaamrisha wamwagilie ndoo ya maji juu ya mkojo wake. Wakati mtoto aliletwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akamkaza kwenye chumba chake ambapo mtoto yule akakojoa kwenye chumba cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akaamrisha yaletwe maji na akayamwaga kwenye mkojo wake. Alinyunyizia juu ya mkono wa mtoto yule bila ya kuosha wala kusugua. Kwa sababu mkojo wa mtoto wa kiume ambaye hajaanza kula chakula, bali ananyonya tu, najisi yake ni khafifu. Inatosha kumwaga maji juu yake yakachirizika pasi na kuosha wala kusugua. Kwa hiyo pindi mtoto anapokojoa juu ya kitanda basi tunatakiwa kuharakisha kuosha.

Lakini tutapaosha vipi ikiwa kitanda hicho hakikukatamana na ardhi kama vile vitanda vikubwa? Kwanza tunatakiwa kuleta sifongo na kupunguza ule mkojo mpaka ukauke. Kisha tunamwaga maji juu ya ule mkojo mara mbili au mara tatu. Baada ya hapo kunakuwa pasafi.

Kuhusu watoto wadogo kimsingi ni kwamba ni wasafi. Hata kama wametoka  chooni kimsingi ni kwamba miguu yao ni misafi. Kwa sababu najisi chooni inakuwa kila sehemu au inakuwa sehemu maalum? Inakuwa sehemu maalum ambapo ni maeneo karibu na kukidhia haja. Sehemu nyingine yote ya chooni ni safi.  Hata yale maeneo karibu na kukidhia haja kukimwagiwa maji juu yake na najisi ikaondoka inasafika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (54) http://binothaimeen.net/content/1223
  • Imechapishwa: 05/09/2019