Kujiunga na kundi la watu walioingia msikitini na kuswali mara nyingine


Swali: Swalah ya Maghrib ilinipita ambapo nikawa nimeswali msikitini peke yangu. Baada ya kumaliza wakaja watu watatu ambapo wakawa wameswali mkusanyiko. Je, niswali pamoja nao na kurudi swalah yangu ili niweze kuandikiwa kwamba nimeswali mkusanyiko?

Jibu: Wewe midhali umeshaswali peke yako umeshatekeleza faradhi. Ukiswali pamoja nao itakuwa ni sunnah. Lakini iwapo watakuja na wewe uko ndani ya swalah, unaweza kuigeuza swalah yako sunnah na ukaingia pamoja nao katika faradhi. Lakini midhali umeshatoa Tasliym mambo kwisha. Ukishatoa Tasliym faradhi imeshaisha. Ukiswali pamoja nao inakuwa swalah ya sunnah. Lakini midhali bado hajatoa Tasliym inafaa kwake kunuia swalah ya sunnah, kisha atoe Tasliym halafu ajiunge pamoja nao ikiwa wakati ni mpana. Lakini hata hivyo lililo bora ni yeye kuikamilisha ikiwa ni swalah ya sunnah kisha ndio ajiunge pamoja nao.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 03/04/2018