Kujitolea futari kwa ajili ya wafungaji


Swali: Kuna baadhi ya jumuiya za kheri ambazo zinakusanya misaada kutoka kwa waislamu kwa lengo la kuandaa chakula cha futari kwa ajili ya mafukara waislamu katika mwezi wa Ramadhaan. Je, yule mwenye kujitolea katika jumuiya hizi anapata thawabu za futari au ni lazima ajitolee futari hiyo mwenyewe?

Jibu: Muislamu akitoa futari kwa ajili ya wafungaji basi anapata thawabu. Hiyo ni swadaqah. Ni mamoja ameitoa mwenyewe au yule mtu ambaye anamwona kuwa ni mwaminifu au jumuiya zenye kuaminika.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/323)
  • Imechapishwa: 02/06/2018