Kujionyesha hakuingii katika matendo ya kidunia

Swali: Kujionyesha kunaingia katika mambo ya kidunia na mtu anahesabiwa kwayo?

Jibu: Matendo ya kidunia hayaingiliwa na kujionyesha. Matendo ya kidunia ni kama mfano wa mambo yaliyohalalishwa kama mfano wa kula, kunywa, kulala na kujenga nyumba kwa mtindo maalum. Isipokuwa ikiwa kama amekusudia kujifakharisha au israfu, hilo ni suala lingine. Kujionyesha kunakuwa katika matendo ya ki-Aakhirah na katika ´ibaadah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (13) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191589#219913
  • Imechapishwa: 16/02/2020