Swali: Ni ipi hukumu ya kujiliza? Ni upi sahihi wa yaliyopokelewa katika hayo?

Jibu: Imepokelewa katika baadhi ya Hadiyth:

“Msipolia basi jilizeni.”[1]

Lakini sijui usahihi wake. Ameipokea Ahmad. Lakini hivi sasa sikumbuki hiyo nyongeza iliyotajwa inayosema:

“Msipolia basi jilizeni.”

Ni kitu kimetangaa kwenye midomo ya wanazuoni. Lakini ni kitu kinachohitajia kutiliwa umuhimu zaidi. Kwa sababu mimi hivi sasa sikumbuki hali ya cheni ya wapokezi wake. Udhahiri ni kwamba asijikakame. Bali ikitokea akali basi apambane na nafsi yake asiwasumbue watu. Bali iwe ni kilio kidogo kisichokuwa na usumbufu kwa kiasi cha uwezo wake.

[1] Ibn Maajah (1327) na (4186).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/347)
  • Imechapishwa: 06/11/2021