Kufunga masiku maalum kwa ajili ya Rajab


Swali: Kuna masiku yanayofungwa ya sunnah katika mwezi wa Rajab. Je, masiku hayo yanakuwa mwanzoni mwake, katikati yake au mwishoni mwake?

Jibu: Hakukuthibiti Hadiyth maalum zinazozunguzia juu ya ubora wa kufunga katika mwezi wa Rajab mbali na yale aliyopokea an-Nasaa´iy, Abu Daawuud na Ibn Khuzaymah akaisahihisha kupitia Hadiyth ya Usaamah aliyesema:

“Ee Mtume wa Allaah! Hatujapatapo kukuona ukifunga mwezi wowote kama unavofanya katika Sha´baan.” Akasema: “Huo ni mwezi ambao watu wengi wanaghafilika nao kati ya Rajab na Ramadhaan. Huo ni mwezi ambao matendo yananyanyuliwa kwa Mola wa walimwengu. Hivyo napenda matendo yangu yanyanyuliwa na mimi ni mwenye kufunga.”

Kilichopokelewa ni Hadiyth zenye kuenea zinazokokoteza juu ya kufunga masiku matatu katika kila mwezi, zengine zinakokoteza kufunga masiku meupe katika kila mwezi; nazo ni tarehe 13, 14 na 15. Hadiyth zengine zinahimiza kufunga mwezi wa Muharram na zengine zinahimiza kufunga jumatatu na alkhamisi. Rajab inaingia katika ueneaji huo.

Kwa hivyo wewe ni mwenye pupa ya kuchagua masiku katika mwezi, basi chagua masiku meupe matatu na jumatatu na alkhamisi. Vinginevyo jambo hili ni pana.

Lakini kufunga masiku kadhaa maalum ya Rajab hatujui kuwa kitendo hicho kina msingi katika Shari´ah.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alifta.net/Fatawa/FatawaChapters.aspx?languagename=ar&View=Page&PageID=335&PageNo=1&BookID=12
  • Imechapishwa: 20/03/2018