Kufanyakazi katika shirika linalouza bidhaa za haramu

Swali: Inajuzu kufanyakazi kwenye shirika linalouza bidhaa za haramu?

Jibu: Hapana. Haijuzu kufanyakazi kwenye shirika linalouza bidhaa za haramu:

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖوَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ

“Shirikianeni katika wema na uchaji Allaah na wala msishirikiane katika dhambi na uadui.” (05:02)

Swali: Mimi sifanyi bidhaa hizi za haramu, ninafanyakazi tu na masanduku na uhasibu.

Jibu: Yote hayo [yana hukumu moja]. Unawatumikia, unawatumikia. Haijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (35) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majid%20-%208%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017