Kufanya kazi na huku mtu anamuiga msomaji wa Qur-aan


Swali: Ni yapi maoni yako kufuatilia kisimo cha Qur-aan Tukufu katika idhaa ya Qur-aan na kusoma pamoja naye na mimi huku niko nafanya kazi?

Jibu: Hakuna ubaya kufuatilia Qur-aan, lakini iwe kwa kunyamaza na isiwe kwa kusoma. Allaah (Subhaanah) Anasema:

وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ

“Na inaposomwa Qur-aan, basi isikilizeni kwa makini na mkae kimya (mzingatie) mpate kurehemewa.” (07:204)

Wewe sikiliza na uzingatie anayosoma msomaji na ustafidi kwayo. Ama kusoma pamoja naye hapana. Sunnah ni kunyama, kuzingatia maana yake na kusikiliza mpaka uweze kustafidi kwa Maneno ya Mola Wako (´Azza wa Jalla). Lakini usisome pamoja na msomaji, nyamaza. Hii ndio Mashru´ah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 26/03/2018