Kufanya Dhwihaar pasina kujua

Swali: Kabla ya kuwa na msimamo na kutafuta elimu mara nyingi nilikuwa natamka Dhwihaar kwa mke wangu wakati kunapotokea baina yetu tofauti. Sikuwa hata najua kama kuna kitu kinachoitwa “Dhwihaar”. Baada ya kutafuta elimu nimejua maana na hukumu yake. Ni ipi hukumu ya Dhwihaar nilizomfanyia mke wangu kabla ya kujua?

Jibu: Dhwihaar, kafara haikatiki kwa ujinga au kusahau. Juu yako una kafara. Hesabu ni mara ngapi ulimfanyia Dhwihaar na utoe kafara kwa kiasi cha unavyoweza. Unatakiwa kutoa mtumwa huru, ikiwa hukuweza funga, ikiwa hukuweza kufunga lisha masikini sitini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (45) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1432-03-24_0.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014