Kufanya darsa na mihadhara katika misikiti ya Ahl-ul-Bid´ah badala ya misikiti ya Ahl-us-Sunnah


Swali: Huyu ni muulizaji kutoka nje ya nchi ambaye anauliza kama inafaa kwao kufanya mihadhara na darsa katika misikiti ya Ahl-ul-Bid´ah na kuacha misikiti ya Ahl-us-Sunnah?

Jibu: Hapana. Fanyeni hayo katika misikiti ya Ahl-us-Sunnah na wale wanaotaka kheri watakujieni katika misikiti ya Ahl-us-Sunnah. Kwa sababu iwapo mtafanya hayo katika misikiti ilio na Bid´ah itakuwa ni kuwashaji´isha juu ya hayo na isitoshe vilevile watatumia hoja kule kuja kwenu kwamba inafaa zile Bid´ah zao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17481
  • Imechapishwa: 24/11/2017