Kuchotwa damu kwa ajili ya kipimo kunaharibu swawm?


Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kuchotwa damu ilihali amefunga katika Ramadhaan?

Jibu: Mfano wa kitu kama hicho hakiharibu swawm. Bali kinasamehewa. Kwa sababu ni katika mambo yanayopelekea katika haja. Sio miongoni mwa mambo yanayofunguza yanayotambulika katika Shari´ah takasifu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/274)
  • Imechapishwa: 29/05/2018