Swali 380: Kuna mwanamke anasema kwamba msichana wake amefariki na hakuweko wakati wa kufa kwake na akazikwa kwenye makaburi yasiyokuwa na wanawake. Maiti wote walioko kwenye makaburi hayo ni wanaume. Je, inajuzu kumzika msichana wake pamoja na wanaume au inafaa kumuhamisha?

Jibu: Inajuzu kuwazika wanawake kwenye makaburi ya wanaume na kinyume chake. Hata hivyo kila maiti azikwe kwenye kaburi lake pekee.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 151
  • Imechapishwa: 02/09/2019