Kubadilisha jina la mababa au mababu lililo na uabudiwa badala ya Allaah

Swali: Ni haki kwa mtu kubadilisha jina la baba yake au babu yake ikiwa uabudiwa wake umenasibishwa kwa asiyekuwa Allaah?

Jibu: Majina ya zamani na ya mtu ambaye kishakufa hayabadilishwi. Akishakufa mwenye nalo halibadilishwi. Ama ikiwa bado yuko hai mtu anaweza kulibadilisha. Ama akishakufa linaachwa kama jinsi lilivyo. Kwa ajili hiyo ndio maana limebaki jina la ´Abdul-Muttwalib.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (28) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-5-25.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014