Swali: Kuna ambao wanaapa kwa haki ya neema tukufu. Je, kuna dhambi kufanya hivo?

Jibu: Neema imeumbwa. Hivyo haijuzu kuapa kwa neema wala haki ya neema.

Swali: Wengine wanaapa kwa kusema “kwa haki ya usiku” au “kwa haki ya siku hii”. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Hali kadhalika [haijuzu]. Siku pia imeumbwa. Hivyo haijuzu kufanya hivyo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (21) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2137
  • Imechapishwa: 09/07/2020