Swali: Inajuzu kuandika baadhi ya Aayah za tukufu tukufu, kama mfano wa “Aayaat-ul-Kursiy”, kwenye vyombo vya chakula na kinywaji kwa lengo la kujitibu?

Jibu: Ni wajibu kwetu kutambua ya kwamba Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall) ni kitukufu zaidi kuliko kukitweza na kukidhalilisha kufikia kiwango hichi. Ni vipi moyo wa muumini utaweze kuhisi vizuri kukifanya Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall) na Aayah kubwa katika Qur-aan ambayo ni Aayaat-ul-Kursiy akaiweka kwenye chombo ambacho anakunywa ndani yake, akaitweza, akaitupa nyumbani na watoto wakacheza nayo? Kitendo hichi hapana shaka kuwa ni haramu.

Ni wajibu kwa yule ambaye yuko na kitu katika vyombo hivi azichane Aayah hizi zilizomo ndani yake. Azipeleke kwa mtengenezaji azichanechane. Asipoweza kufanya hivo ni wajibu kwake kuzichimbia sehemu safi na kuzifukia. Ama kuzibakiza hali ya kutwezeka na kudhalilishwa zikawa zinakunyiwa na kuchezewa na watoto, hakika kujitibu kwa Qur-aan kwa njia kama hii haikuthibiti kutoka kwa as-Salaf as-Swaalih (Radhiya Allaahu ´anhum).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (01/109-110)
  • Imechapishwa: 10/06/2017