Kuacha kufunga kwa sababu ya kazi ni haramu

Swali: Ni yepi maoni yako kwa yule ambaye kazi yake ni ngumu na anapata uzito wa kufunga. Je, itafaa kwake kuacha kufunga?

Jibu: Naona kuwa kula kwake kwa sababu ya kazi ni haramu na haijuzu. Ikiwa hawezi kukusanya kati ya kufanya kazi na kufunga basi achukue likizo katika Ramadhaan ili aweze kufunga katika Ramadhaan. Kwa sababu kufunga Ramadhaan ni nguzo miongoni mwa nguzo za Uislamu. Haifai kukiukwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 455
  • Imechapishwa: 29/04/2020