Kuna aina mbili za viongozi:

1- Viongozi wa uongofu.

2- Viongozi wa upotevu.

Kiongozi wa wakanushaji ni Fir´awn. Viongozi wa wathibitishaji ni Muhammad, Ibraahiym, Muusa na Mitume wengine waliobakia huu ndio ulikuwa mwenendo wao. Anayemkanushia Allaah majina na sifa Zake basi huyo anamfuata Fir´awn. Anayemthibitishia Allaah majina na sifa Zake basi huyo anamfuata Muhammad, Ibraahiym na Muusa (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam).

Mwandishi (Rahimahu Allaah) anasema kuwa Fir´awn ndio kiongozi wa wakanushaji ambaye alimkanusha Mola Mtukufu ambaye amesimamisha mbingu, ardhi na kila kitu kwa maamrisho Yake. Badala yake akasema kuwa yeye ndiye mola mkuu wa watu. Upande mwingine wakanushaji ambao ni Jahmiyyah wamekanusha Allaah kuwa na majina na sifa. Wamesema kuwa Allaah hana usikizi, uoni, ujuzi, uwezo, hasifiwi kuwa juu, hasifiwi kuwa amelingana, hasifiwi kuwa anaumba na kuruzuku. Hawakuthibitisha jina wala sifa yoyote. Maelezo haya ni maelezo ya kitu kisichokuwepo. Kadhalika hawa wakanamungu wanasema juu ya mungu wao ya kwamba hana usikizi, uoni, uwezo, hayuko chini, hayuko juu, hayuko upande wa kulia wala wa kushoto, haonekani, hapandi wala hashuki, haumbi, haruzuku, hahuishi wala hafishi na wala hasifiwi kwa sifa yoyote ile. Huwezi unakanielezea juu ya kitu kisichopatikana zaidi ya maelezo haya.

Wakanushaji hawa kiongozi wao ni Fir´awn. Kwa kuwa yeye ndiye ambaye alikanusha kuwepo kwa Mola na akasema yeye ndiye mola wao mkuu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qaa´idah al-Marraakushiyyah, uk. 80
  • Imechapishwa: 30/04/2020