Kinachozingatiwa ni yaliyothibiti kutoka kwa mwenye kuigwa

Swali: Je, Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) alikuwa na dalili ya kukata ndevu zenye kuzidi juu ya ngumi au hiyo ilikuwa ni Ijtihaad yake?

Jibu: Ni Ijtihaad yake. Ni Ijtihaad yake Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) hali ya kutegemea Aayah ya al-Fath:

مُحَلِّقِينَ رُءُوسَكُمْ وَمُقَصِّرِينَ

”… hali ya kuwa mmenyoa vichwa vyenu na wenye kupunguza.”[1]

Kwa ajili hiyo hutomuona Ibn ´Umar anafanya hivo kinyume na msimu wa hajj. Alikuwa anafanya hivo katika msimu wa hajj kwa ajili ya kutendea kazi Aayah. Kwa ajili alikuwa anaona kuwa (وَ) ni ya kukusanya. Kwa hiyo ni lazima mtu anyoe na kupunguza vyote pamoja. Akinyoa kichwa chake ni kitu gani kinachobakia kupunguzwa? Ni ndevu. Kwa hiyo alikuwa akikusanya yote mawili kwa ajili ya kutendea kazi Aayah. Hiyo ni Ijtihaad yake (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Vilevile imepokelewa kutoka kwa baadhi ya Maswahabah. Mazingatio ni yale yaliyothibiti kwa ambaye ni kiigizo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ilikuwa inajulikana kuwa anasoma  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kutikisika kwa ndevu zake kwa nyuma yake.

[1] 48:27

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Kariym bin ´Abdillaah al-Khudhwayr
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://saif.af.org.sa/sites/default/files/01_36.mp3
  • Imechapishwa: 18/09/2022