Kinachowalazimu wanaochelewesha kulipa siku zao za Ramadhaan


Swali: Mwanamke akila siku moja ya Ramadhaan na akachelewa kuilipa mpaka akaingiliwa na Ramadhaan nyingine – ni kipi kinachomlazimu hivi sasa?

Jibu: Ikiwa alichelewesha kulipa kwa sababu ya udhuru mpaka akaingiliwa na Ramadhaan ya pili hakuna kinachomlazimu isipokuwa kulipa baada ya kumaliza hiyo Ramadhaan ya pili. Ama ikiwa alichelewesha pasi na udhuru basi analazimika kufanya mambo mawili:

1- Kulipa. Ni lazima kwake kulipa baada ya Ramadhaan aliyomo.

2- Kulisha masikini kwa kila siku moja. Hii ni kafara kwa kule kuchelewesha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl (07) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/charh-el-osol-el-thalatha/charh-fwzan/07.mp3
  • Imechapishwa: 25/01/2019