Kila siku anatokwa na matone kadhaa baada ya kukojoa

Swali: Baada ya kumaliza kukojoa nasubiri kiasi kidogo utoke mkojo wote kisha baada ya hapo naosha dhakari. Wakati mwingine natumia mawe. Halafu baada ya muda kidogo, kama takriban robo saa au chini ya hapo, napata kitu kidogo katika mkojo kama tone mbili au tatu. Nifanye nini pamoja na kuzingatia kwamba hili ni jambo ambalo linajitokeza kwa kuendelea?

Jibu: Namuomba Allaah amponye haraka. Sioni kama kuna njia nyingine isipokuwa asubiri mpaka mkojo umalizike kabisa. Hali ikipelekea kutoka hiyo sehemu ya kukidhia haja na ukapiga baadhi ya hatua… kwa sababu akipiga baadhi ya hatua huenda ukatoka ule mkojo ulobaki.

Namnasihi ndugu huyu aende kwa madaktari wataalam. Kwa sababu Allaah hakuteremsha magonjwa isipokuwa pia kateremsha dawa yake. Huenda akapata dawa ambayo Allaah akamponya kwayo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (54) http://binothaimeen.net/content/1231
  • Imechapishwa: 16/09/2019