Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye kila Ramadhaan anashika mimba na hakuweza kulipa siku anazodaiwa?

Jibu: Ni wajibu kwa mwanamke huyu anayezaa katika Ramadhaan kulipa idadi ya masiku anayodaiwa baada ya Ramadhaan. Akichelewesha kulipa mpaka kukaingia Ramadhaan nyingine bila ya udhuru wa Kishari´ah basi ni wajibu kulipa pamoja na kulisha masikini kwa kila siku moja atakayofunga. Ikiwa kuchelewesha huko ni kwa udhuru basi ni wajibu kulisha idadi ya yale masiku anayodaiwa peke yake.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/368)
  • Imechapishwa: 23/06/2017