Kila mwaka kampuni kufanya sherehe kwa ajili ya wafanyakazi

Swali: Kuna mtu yuko na kampuni na kumeshapita muda mrefu ambapo anataka kusherehekea ili kuonyesha zile kazi alizofanya? Unamnasihi nini ju ya hilo? Afanye au asifanye? Ni ipi hukumu ya kumpongeza juu ya hilo?

Jibu: Naona asifanye. Kwa sababu nachelea asije kuchukulia hilo kuwa sikukuu ambapo kila kunapotimia mwaka basi anafanya sherehe. Allaah hakuujaalia Ummah huu sikukuu ya kusherehekea isipokuwa ´Iyd-ul-Fitwr na ´Iyd-ul-Adhwhaa´ na siku ya ijumaa ambayo ni sikukuu ya wiki. Siku hii ina sifa zake za kipekee. Lakini sikukuu ya Adhwhaa´ na Fitwr ndani yake inafaa kufanya michezo na kupiga dufu mambo ambayo hayafai kufanywa katika mnasaba mwingine. Hizi ndio sikukuu tatu za Kiislamu. Haifai kwa mtu kufanya sikukuu zengine mbali na sikukuu hizi mbili.

Lakini ni sawa mtu anapotimiza mwaka na mambo yake ya biashara yakapitika vizuri akamshukuru Allaah (Ta´ala) na akamhimidi kwa hilo. Bali haya ni miongoni mwa mambo yanayotakikana. Ama kufanya sikukuu au sherehe haifai.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (58) http://binothaimeen.net/content/1335
  • Imechapishwa: 11/11/2019