Kila jina la Allaah limebeba sifa


Swali: Je, yapo miongoni mwa majina ya Allaah yanayokusanya jina na sifa?

Jibu: Kila jina la Allaah linatokana na dhati na sifa. Mpaka neno (الله) linajulisha dhati na uungu. Yeye (Subhaanah) ndiye Mungu anayeombwa, akaabudiwa, kunyenyekewa na kustahiki kuabudiwa kwa aina zote. Allaah (Subhaana) amesema:

ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ هُوَ الْبَاطِلُ

“Hivyo ni kwa kuwa Allaah ndiye wa haki na kwamba vile wanavyoomba badala Yake ndiyo batili.”[1]

[1] 22:62

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (09/74)
  • Imechapishwa: 09/07/2021