Swali: al-Ahdal anasema kwamba yule mwenye kutenda madhambi hadharani anaonelea kuwa dhambi hiyo ni halali na kwamba dalili ya hilo ni maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):

“Ummah wangu wote ni wenye kusamehewa siku ya Qiyaamah isipokuwa wale wenye kudhihirisha madhambi.”

Jibu: Je, mnazingatia kuwa ni kufuru kutokana na kanuni ya dalili za Ahl-us-Sunnah ya kwamba wanaafisa wanachukua ushuru kutoka watu au mwanamke kutoka hali ya kuwa amevaa lakini bado yuko uchi?

Ikiwa unapokea nasaha zangu ninakunasihi wende kwa Shaykh Ibn Baaz na Shaykh al-Albaaniy. Nenda na kitabu chako na piga magoti, wasogelee na ufaidike katika elimu yao. Sasa umekuwa Khaarijiy, Mu´taziliy na Shiy´iy! Ni Mu´tazilah na Shiy´ah ndio huwachochea watu kufanya uasi kwa watawala.

Ama kuhusu Ahl-us-Sunnah, wanazihifadhi damu za Waislamu na wanajitenga mbali na fitina.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 160
  • Imechapishwa: 22/04/2015