Khawaarij na Mu´tazilah ndio wenye kupinga hodhi


Kuna mapote yaliyopinga kuwepo kwa hodhi ikiwa ni pamoja na Khawaarij na baadhi ya Mu´tazilah.

Ama kuhusiana na Ahl-ul-Haqq ambao ni Ahl-us-Sunnah wanaamini hodhi na ni haki ambayo ni wajibu kuiitakidi na kuiiamini. Dalili juu ya kuthibiti kwa hodhi ni nyingi na zimefikia kiasi cha Hadiyth iliyopokelewa kwa mapokezi mengi [Mutawaatir]. Imepokelewa na Maswahabah thelathini na zaidi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/305)
  • Imechapishwa: 21/05/2020