Swali: Inafaa kwa Khatwiyb kunywa wakati wa Khutbah kama alivyokunywa maziwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa salalm) siku ya ´Arafah?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa salalm) alikuwa hatoi Khutbah, alikuwa ameketi juu ya mnyama wake. Lakini hata hivyo hakuna ubaya kwa Khatwiyb kunywa akihitajia kufanya hivo na huku anatoa Khutbah. Kilichokatazwa ni wakati wa swalah ndio haifai kunywa ilihali mtu anaswali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (19) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdtfq-22011435-01.mp3
  • Imechapishwa: 15/12/2019