Khatwiyb akiwajuzishia wafanya kazi kula na badala yake kutoa chakula

Swali: Nimemsikia Khatwiyb katika maimamu wa misikiti katika Khutbah ya pili katika Ramadhaan iliyobarikiwa akimjuzishia mfanya kazi aliyelazimika na wakati huohuo akawa hana kazi nyingine mbali na hii kwamba inatosha kutoa chakula kumlisha masikini kwa kila siku moja ya Ramadhaan. Je, haya yana dalili sahihi kutoka katika Qur-aan na Sunnah?

Jibu: Haijuzu kwa ambaye swawm inamuwajibikia kula mchana wa Ramadhaan kwa sababu tu eti ni mfanya kazi. Lakini akipata uzito mkubwa wenye kumpelekea kula mchana wa Ramadhaan basi atakula kiasi cha kuondosha uzito kisha baada ya hapo atajizuia mpaka wakati wa kuzama kwa jua. Jua likishazama atakula pamoja na wengine na atalipa siku hiyo aliyokula. Fatwa uliyotaja si sahihi.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah al-Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daa’imah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Ladjnah ad-Daa’imah (4157)
  • Imechapishwa: 27/04/2020