Swali: Nimepata kazi kwenye benki inayofanya mu´amala wa ribaa. Je, inafaa kufanya kazi hapo?

Jibu: Hapana, usifanye kazi hapo. Benki zinafanya mu´amala wa ribaa. Ukifanya hapo basi umeshirikiana nao katika madhambi na uadui. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wenye kula ribaa, wenye kuitoa, wenye kuiandika na wenye kuishuhudia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/18073
  • Imechapishwa: 14/07/2019