Katika swalah ya ´Iyd imamu akhutubu akiwa juu ya mimbari?


Swali: Je, imesuniwa kwa imamu kukhutubu akiwa juu ya mimbari katika swalah ya ´Iyd?

Jibu: Ndio. Baadhi ya wanachuoni wanaonelea kuwa ndio Sunnah. Kwa sababu katika Hadiyth ya Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwakhutubia watu halafu akaeleza:

“Kisha akateremka na kuwaendea wanawake.”

Wametumia hoja kwamba kuteremka hakukuwi isipokuwa kutokea sehemu iliyo juu. Hivi ndivo wanavofanya watu.

Wanachuoni wengine wanaonelea kuwa bora ni kutoa Khutbah bila mimbari. Jambo hili lina wasaa ndani yake – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawa (16/250)
  • Imechapishwa: 14/06/2018