Swali: Katika darsa ya jana umesema kuwa kupata idhini ya wazazi wawili ni wajibu kwa yule anayetaka kwenda katika Jihaad. Mtu akienda bila ya kupata idhini yao na kusema kuwa anasamehewa madhambi yake kwa lile tone la kwanza tu la damu – kama alivyosema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – je, mtu kama huyu anasamehewa madhambi yake kweli?

Jibu: Tukisema kuwa kuwataka idhini ni wajibu itakuwa kwenda kwake ni kitendo cha haramu. Katika hali hii haiwi ni Jihaad yenye kukubaliwa. Anachotakiwa ni yeye kuwakinaisha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (23)
  • Imechapishwa: 09/01/2019