Kamati ya wanachuoni wakubwa Saudi Arabia kuhusu Salafiyyah

Swali 188: Salafiyyah ni nini? Ni yepi maoni yenu juu yake?

Jibu: Salafiyyah ni unasibisho kwa Salaf ambao ni Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), maimamu wa uongofu katika wale wa karne tatu wa mwanzo (Radhiya Allaahu ´anhum) ambao wameshuhudiwa ubora na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale aliposema:

“Watu bora ni wa karne yangu, kisha wale watakaofuatia, kisha wale watakaofuatia. Kisha watakuja watu ushuhuda wa mmoja wao unatangulia kiapo chake na kiapo chake ushuhuda wake.”

Ameipokea Ahmad katika “al-Musnad” yake, al-Bukhaariy na Muslim.

Salafiyyuun ni wingi wa Salafiy. Ni unasibisho wa Salaf. Maana yake imekwishatangulia kwamba ni wale wenye kufuata mfumo wa Salaf ambao wanafuata Qur-aan na Sunnah na kulingania katika viwili hivyo na kuvitendea kazi. Kwa sababu hiyo ndio maana wakawa ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 403
  • Imechapishwa: 05/01/2020