Kama mtu amelazimika kwenda kwa wachawi na wapiga ramli


Swali: Ni ipi hukumu ya kwenda kwa wachawi na makuhani kwa lengo la matibabu mtu akiwa amelazimika kufanya hivo?

Jibu: Haijuzu kwenda kwa makuhani, wachawi na waganga wala kuwauliza. Bali ni lazima kuwazindua, kuwachukulia hatua na kuwakataza. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote atakayemwendea mpiga ramli au kuhani akamsadikisha kwa aliyoyasema, basi hakika ameyakufuru yale aliyoteremshiwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Aliulizwa kuhusu makuhani ambapo akasema:

“Msiwaendee.”

Makuhani wanadai kujua mambo yaliyofichikana kwa msaada wa mashaytwaan wao. Kwa hivyo haijuzu kuwaendea makuhani, wapiga ramli wala kuwauliza kitu. Bali ni lazima kuwakemea na kuwaadabisha ili wasirudi katika kitu kama hicho. Lakini aende kwa watu wa kheri wanaotambulika kufanya matabano yanayokubalika katika Shari´ah wawafanyie matabano.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (09/259)
  • Imechapishwa: 10/07/2021