Ni makosa kusikiliza kanda bila ya kujua ni nani mzungumzaji. Kuna kanda za watu wasiojulikana. Haifai ukajiaminisha. Kabla ya kusikiliza unatakiwa kwanza kuuliza kama mzungumzaji ni katika Ahl-us-Sunnah na kama inafaa kusikiliza kanda zake.

Baadhi ya watu mali kwao ni yenye hadhi kubwa pamoja na kuwa wanaichukulia dini yao usahali. Dini yao kwao ni kitu rahisi; wanamsikiliza mtu ni mtu na wanakaa na yeyote yule. Mambo sivyo inapokuja katika mali zao. Ni wenye kuipa hadhi. Ni kwa nini basi angalau msiitazame dini yenu kuwa na hadhi kama hiyo? Ni kipi chenye haki zaidi ya kuangaliwa na kuhifadhiwa? Dini au mali? Dini. Hawaipi uzito dini, wanaipa uzito mali. Wanauliza kuna tatizo gani mtu akimsikiliza mtu fulani. Ikiwa mzungumzaji ni jitu la Bid´ah basi kuna kila aina ya shari.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.com/Dars-14107
  • Imechapishwa: 18/09/2020