Jini kumwingia mwanaadamu na kutamka ndani ya mwili wake


Swali: Je, ni sahihi ya kwamba jini linaweza kumwingia mtu na likamfanya akaongea kwa sauti yake?

Jibu: Ndio. Jini linaweza kumwingia mtu. Likamwingia kwa sifa maalumu na likamfanya mtu akatamka kwamambo, hujulikana sauti ya jini na ya sauti ya mtu. Hili ni jambo hutokea tangu zamani mpaka sasa. Hali kadhalika mwendawazimu. Aliyeingiwa na jini na mwendawaz-imu hutamka kwa maneno: “Nipeni kadhaa”, “Fanyeni kadhaa” n.k., kwa sauti wanayoisikia watu isiyokuwa sauti ya mwanaadamu. Hili ni jambo ambalo hutokea, na mwenye kupinga hili kakosea. Jini humwingia mtu na kwa hili anakuwa kama mwendawazimu akili zake zinatoweka. Linapomtoka (jini hilo) na kutengana nae, akili zake hurudi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 30/03/2018