Swali: Je, mtu wa Bid´ah anapewa udhuru akiwa ni mjinga?

Jibu: Haifai kwa mtu kufanya jambo isipokuwa mpaka ajue kuwa kitu hicho kimesuniwa. Akiwa sio msomi basi awaulize wanachuoni. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

“Basi waulizeni watu wenye ukumbusho ikiwa nyinyi hamjui.” (16:43)

Mtu ambaye amefanya jambo hilo kwa ujinga aelekezwe na abainishiwe kwamba kitendo hicho ni katika Bid´ah na kwamba ni lazima kukiacha. Aking´ang´ania na akaendelea juu yake anasifiwa kwamba amefanya Bid´ah hii. Lakini kama nilivyotangulia kusema kwamba Bid´ah haziko katika kiwango kimoja. Bid´ah zinatofautiana kama ambavo dhambi kubwakubwa na maasi yanatofautiana.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bid´at-ul-Mawaalid wa mahabbat-in-Nabiyy http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=36078
  • Imechapishwa: 10/11/2019