Swali: A) Je, inajuzu kuogelea katika Ramadhaan?

B) Mtu akiumia mkononi mwake au mguuni mwake katika Ramadhaan swawm yake inaharibika?

C) Mtu akichukua manukato na akayaweka mwilini kwake swawm yake inaharibika?

D) Je, matukano na maapizo yanaharibu swawm?

E) Je, vipumbazo na michezo inajuzu mchana wa Ramadhaan?

Jibu: A) Inajuzu kuogelea mchana wa Ramadhaan. Lakini inatakiwa kwa mfungaji achunge maji yasiingie tumboni mwake.

B) Mtu akiumia mkononi mwake au mguuni mwake na akatokwa na damu hakumfunguzi.

C) Mtu akijitia manukato mwilini mwake au kwenye mavazi yake hakumfunguzi. Lakini akijiweka nayo puani kunamfunguza.

D) Matusi na maapizo hayafai si kwa mfungaji wala mtu mwengine. Lakini ni haramu zaidi kwa mfungaji. Ikitokea akafanya hivo ilihali amefunga hakumfunguzi. Lakini hata hivyo anapata dhambi.

E) Mfungaji anatakiwa aichunge nafsi yake kutokamana na vipumbazo na michezo na badala yake ajikurubishe kwa Allaah kwa kutekeleza maamrisho Yake na kujiepusha na makatazo Yake. Anatakiwa ajiepushe na kila jambo linalomfanya kuwa mbali na Allaah na kumuabudu. Ni mamoja iwe lengo au njia.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/282)
  • Imechapishwa: 14/06/2017