Mu´tazilah, Haruuriyyah na Jahmiyyah wanadai kuwa Allaah (´Azza wa Jall) yuko kila mahali. Hilo linapelekea ya kwamba Yuko tumboni mwa Maryam na kwenye mashamba ya mitende na kwenye vyoo. Fikira kama hiyo inakwenda kinyume na dini. Ametakasika Allaah kuliko kukubwa kutokamana na wanayoyasema.

Wanatakiwa kuambiwa, ikiwa hakulingana juu ya ´Arshi kwa maana ambayo ni maalum kwa ´Arshi pasi na chengine, kama walivyosema wanachuoni na wapokezi wa maelezo, na Allaah (´Azza wa Jall) akawa kila mahali. Basi katika hali hiyo Yuko chini ya ardhi ambayo imefunikwa na mbingu. Akiwa chini ya ardhi na ardhi ikiwa juu Yake na mbingu iko juu ya ardhi, hivyo hilo linapelekea nyinyi kusema kuwa Allaah yuko huko chini kabisa na vyengine vyote viko juu Yake na kwamba Yuko juu kabisa na vyengine vyote viko chini Yake. Kwa hayo Yeye yuko chini ya vile vilivyoko juu Yake na juu ya vile vilivyoko chini Yake. Ni jambo lisilowezekana na ni mgongano – Allaah ametakasika kutokamana na uongo wao!

  • Mhusika: Imaam Abul-Hasan ´Aliy bin Ismaa´iyl al-Ash´ariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ibaanah, uk. 443
  • Imechapishwa: 15/04/2017