Jamaa´at-ut-Tabliygh na wenye kutoka pamoja nao wayazingatie haya

Swali: Mume wangu husafiri wakati wa likizo na akaiacha familia yake wakiwemo watoto na wasichana wanapotea. Ni ipi nasaha zako kwake na kwa watu mfano wao?

Jibu: Nasaha zangu kwake na kwa watu mfano wake ni kwamba: kubaki kwao pamoja na familia zao ni kheri kwao kuliko kusafiri ikiwa wanahitajia kuwaangalia. Kwa sababu wakibaki basi wametekeleza wajibu wao ambao Allaah kawawajibishia pale aliposema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ

“Enyi walioamini! Jikingeni nafsi zenu na ahli zenu kutokamana na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe.” (66:06)

Kadhalika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewawajibishia jambo hilo pale aliposema:

“Mwanaume ni mchungi juu ya familia yake na ataulizwa juu ya kile alichokichunga.”

Ama ikiwa wataendelea juu ya yale waliyomo katika matendo mema, basi ana haki ya kusafiri. Lakini haifai kwake akawaacha nyuma mwezi mmoja, nusu mwezi na kadhalika isipokuwa kwa dharurah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (65) http://binothaimeen.net/content/1463
  • Imechapishwa: 12/01/2020